AZERBAIJAN

Azerbaijan yatangaza kifo cha mmoja wa wanajeshi wake huko Nagorno-Karabakh

Wanajeshi wa  Azerbaijan wakiwa katika jimbo la  Nagorno-Karabakh
Wanajeshi wa Azerbaijan wakiwa katika jimbo la Nagorno-Karabakh AFP

Wizara ya Ulinzi ya Azerbaijan imetangaza Jumatatu kwamba mwanajeshi wake mmoja ameuawa katika shambulio katika eneo la Nagorno-Karabakh.

Matangazo ya kibiashara

Eneo hilo lilikuwa  chanzo cha mzozo mpya kati ya vikosi vinavyotaka kujitawala kutoka Armenia na vikosi vya Azerbaijan.

Mkataba wa kusitisha mapigano ulianza kutumika Novemba 10 baada ya wiki sita za mapigano.

Mgogoro huo uliwauwa maelfu ya watu, kusababisha wengi kupoteza makazi na kutishia kuitumbukiza kanda hiyo nzima katika vita.