UINGEREZA-EU

Mabalozi wa Umoja wa Ulaya waidhinisha mkataba kati ya EU na Uingereza

Bendera za Umoja wa Ulaya
Bendera za Umoja wa Ulaya AFP

Mabalozi kutoka mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya kwa kauli moja, wameidhinisha mkataba uliokubaliwa kati ya viongozi wa Umoja huo na Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja, wakati huu mkataba huo unapotarajiwa kujadiliwa na kupigiwa kura na wabunge nchini Uingereza siku ya Jumatano, kabla ya kuwa sheria kuanzia Januari tarehe Moja.

Hata hivyo, wabunge wa Umoja wa Ulaya, wanatarajiwa kuujadili na kuupigia kura, mkataba huo mapema mwaka 2021.

Mkataba huo, unaeleza namna Uingereza itakavyoshirikiana na mataifa ya Umoja wa Ulaya kuhusu masuala ya biashara, safari za watu miongoni mwa mambo mengine baada ya nchi hiyo kujiondoa rasmi kwenye umoja huo ifikapo mwisho wa mwaka huu.

 

Mkataba huo wenye kurasa 1,246 inamalizika karibu miaka 50 ya uanachama wa Uingereza kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.