UFARANSA

Covid-19 Ufaransa: Hali yaendelea kuwa mbaya, Macron akabiliwa na shinikizo kutoka kwa Mameya

Emmanuel Macron rais wa Ufaransa
Emmanuel Macron rais wa Ufaransa Christophe Petit Tesson, Pool via AP

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajia kuongoza kikao cha baraza la ulinzi wa afya, siku mbili kabla ya hotuba yake Desemba 31, wakati mameya kadhaa wakitaka kuimarishwa kwa hatua za kiafya.

Matangazo ya kibiashara

Kikao hiki kitafanyika huko Brégançon kunako patikana makaazi yake ambako alikuwa akiishi kwa siku kadhaa baada ya kujiweka karantini kufuatia kuambukizwa virusi vya Corona.

Kikao hiki cha baraza la ulinzi wa Afya ambacho kitafayika kwa njia ya video kitaangazia kwa kina kuhusu ugonjwa hatari wa Covid-19.

Emmanuel Macron ambaye ataongoza kikao hiki, Waziri Mkuu na mawaziri husika watatathmini hali ya afya siku wakati kampeni ya chanjo imeanza hivi punde tu nchini Ufaransa na kusambaa kwa virusi kumeendelea kuzua wasiwasi mkubwa nchini humo.

Maafisa kadhaa waliochaguliwa katika maeneo mbalimbali huko Grand Est na Alpes-Maritimes hasa, ambapo janga hilo limefikia viwango vya kutisha, wameomba serikali kuchukua hatua haraka ikiwa ni pamoja na vizuizi vya nyumbani au kuongeza kasi ya chanjo.

Mameya wanaomba maamuzi ya haraka bila kusubiri kuanza kwa mwaka wa shule.

Kwa upande wa Ikulu ya Elysee wanasema bado ni haraka mno kuchukua hatua hizo, huku ikiwataka raia kusuburi hadi mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2021, labda Januari 7, baada ya kikao cha baraza la mawaziri.