UINGEREZA-CORONA

Uingereza: Chanjo milioni 2 ya corona kutolewa kila wiki kwa kuepuka wimbi jipya

Chanjo iliyotengezwa na kampuni ya  Pfizer na BioNTech.
Chanjo iliyotengezwa na kampuni ya Pfizer na BioNTech. JOEL SAGET / AFP

Uingereza inapaswa kutoa chanjo kwa watu milioni mbili kila wiki ili kuepuka mlipuko wa tatu wa janga la Corona, kulingana na matokeo ya utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha London.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya vifo 71,000 vilivyotokana na janga hilo vimerekodiwa nchini Uingereza, ambapo zaidi ya watu milioni 2.3 wameambukizwa virusi hivyo, kulingana na takwimu za shirika la habari la REUTERS .

"Ili kuepukana na mlipuko mpya wa janga la Corona kuna ulazima wa kuchukuliwa masharti mapya ya kudhibiti kusambaa kwa Corona nchini kote Uingereza, shule zinapaswa kufungwa mnamo mwezi Januari na watu milioni mbili wanapaswa kupewa chanjo kwa wiki, " kimeandika Chuo Kikuu cha London, London School of Hygiene and Tropical Medicine (LSHTM).

"Kwa kukosekana kwa kupelekwa kwa chanjo ya kutosha, kesi (za maambukizi), watu kulazwa hospitalini au kulazwa katika wodi za wagonjwa mahututi mnamo 2021 zinaweza kuzidi zile za mwaka 2020", LSHTM kimeongeza katika hitimisho lake.

Uingereza mapema mwezi huu ilikuwa nchi ya kwanza ya Magharibi kuzindua kampeni yake ya chanjo ya Corona, kwa kutumia chanjo iliyotengenezwa na maabara ya Pfizer na BioNTech.