UINGEREZA-EU

Brexit: Uingereza na Uturuki zasaini mkataba wa kibiashara

Rais wa Uturuki  Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Adem ALTAN / AFP

Uingereza imetangaza kutia saini kwenye mkataba wa kibiashara na Uturuki. Mkataba huo utawezesha kupanua mipangilio ya forodha iliyopo ndani ya mfumo wa Umoja wa Ulaya baada ya Januari 1, pamoja na matumaini ya kufikia baadaye mkataba kamili wa biashara huria.

Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo ulitiwa saini na pande mbili katika mkutano kwa njia ya video kati ya Waziri wa Uingereza wa Biashara ya Kimataifa Liz Truss na mwenzake wa Uturuki Ruhsar Pekcan.

Aidha, utawezesha makampuni ya Uingereza kuendelea kufanya biashara na Uturuki katika mazingira sawa kama kabla ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya (Brexit).

Pande hizo mbili pia zimekubaliana kujaribu kufikia mkataba "kabambe zaidi" katika siku zijazo. Uingereza sasa inaonekana kama bingwa wa biashara huria baada ya Brexit.

Idadi kubwa ya mikataba 62 ya biashara iliyosainiwa na nchi tofauti inaongeza tu mipango iliyopo na Umoja wa Ulaya. Kuhusu mazungumzo na Marekani, hadi sasa Washington haijatoa chochote licha ya ahadi za Donald Trump, ambaye sasa anaondoka mamlakani.