URUSI

Urusi yamwita balozi wa Uingereza na yaongeza vikwazo

Alexei Navalny mwanasiasa wa Urusi
Alexei Navalny mwanasiasa wa Urusi AP Photo/Pavel Golovkin

Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi imesema imemwitisha balozi wa Uingereza huko Moscow na kuongeza majina kwenye orodha ya wawakilishi wa Uingereza waliopigwa marufuku kuingia katika nchini humo kwa kujibu vikwazo vya London katika kesi ya Alexei Navalny.

Matangazo ya kibiashara

Urusi haijatoa majina ya maafisa wa Uingereza, wanasiasa na watu wengine waliochukuliwa vikwazo lakini imewataja kuwa wanahusika katika utekelezaji wa vikwazo dhidi yake.

Moscow imeongeza kuwa imempa Deborah Bronnert, balozi wa Uingereza nchini Urusi, barua inayoelezea msimamo wake.

Kulingana na Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi, Moscow ililazimika kujibu vikwazo vilivyochukuliwa na Uingereza mnamo mwezi Oktoba, ambapo Urusi inasema kuwa vikwazo dhidi yake havikubaliki na havieleweki.

Uingereza na Umoja wa Ulaya mnamo mwezi Oktoba waliweka vikwazo dhidi ya maafisa wakuu wa Urusi ambao ni washirika wa karibu wa Vladimir Putin, kwa jukumu lao la madai ya kumpa sumu Alexey Navalny Agosti iliyopita.

Alexei Navalny, ambaye ni kiongozi wa upinzani na mkosoaji mkubwa wa utawala wa Putin, kwa sasa anapumzika nchini Ujerumani baada ya kupewa sumu nchini Urusi na aina ya Novichok.

Urusi imeendelea kukaniusha madai hayo wakati Uingereza na nchi zingine za Magharibi zilitaka Moscow kujibu kesi hiyo.

Kremlin imesema haioni ushahidi wowote wa kupewa sumu Alexei Navalny na rais wa Urusi Vladimir Putin amebaini kwamba njia ya tukio hilo iliyowasilishwa huko Magharibi ilikuwa sehemu ya njama iliyoungwa mkono na Marekani kwa jaribio la kudhalilisha Urusi.