MARKANI-AUSTRALIA

Hatima ya Julian Assange kujulikana Jumatatu

Julian Assange akiwa nchini Uingereza
Julian Assange akiwa nchini Uingereza REUTERS/Simon Dawson

Mahakama ya Uingereza inatarajia kutoa uamuzi wake juu ya kutumwa au la kwa Assange nchini Marekani, baada ya kushtumiwa makosa mbalimbali nchini humo

Matangazo ya kibiashara

Julian Assange anasubiri uamuzi wa jaji wa Uingereza ikiwa atakubali ombi la Marekani la kukabidhiwa kwake nchini humo.

Marekani inamshutumu mwanzilishi wa WikiLeaks makosa ya ujasusi na njama ya kuchapisha kwenye tovuti yake mamia ya maelfu ya nyaraka za siri zinazohusu jeshi la nchi hiyo mnamo 2010.

Ikiwa atakabidhiwa nchi ya Marekani, kisha akapatikana na hatia ya mashtaka dhidi yake, Julian Assange, mwenye umri wa miaka 49, anaweza kuhukumiwa miaka 30 hadi miaka 40 jela, mawakili wake wanasema.

Julian Assange ni mhariri wa mtandao wa Wikileaks aliyesimamia uchapishwaji wa nyaraka kadhaa za siri kutoka serikali kadhaa duniani.

Assange anatakiwa nchini Marekani na Sweden akihusishwa na uchunguzi wa masuala ya uhalifu.

Kwa kuhofia kukamatwa na kupelekwa kwenye nchi hizo, Assange aliomba na kupatiwa hifadhi ya kisiasa na Equador na tangu mwaka 2012 amekuwa akiishi kwenye ubalozi wa nchi hiyo mjini London, Uingereza.