UJERUMANI

Ujerumani yarefusha muda wa kufunga shughuli za kimaisha hadi Januari 31 kudhibiti kuenea kwa Corona

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel Fabrizio Bensch/pool photo via AP

Hatua zilizopitishwa na Ujerumani katikati ya mwezi Desemba na kutumika hadi Jumapili ijayo zitaendelea kutumika hadi mwishoni wa mwezi huu, serikali kuu ya Ujerumani imesema.

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kurefusha muda wa kufunga shughuli mbali mbali ili kudhibiti janga la kusambaa virusi vya Corona nchini Ujerumani inatarajiwa kutangazwa rasmi leo Jumanne baada ya mkutano kati ya Kansela Angela Merkel na mawaziri wakuu wa majimbo yote 16 ya nchi hii.

Ili kupambana kwa ufanisi zaidi dhidi ya viwango vya maambukizi ambavyo bado ni vikubwa mno, mfumo wa sasa utaimarishwa, imeongeza serikali ya Ujerumani.

Kufikia sasa hatua ya kufunga maduka,shule na huduma nyingine kote nchini Ujerumani tangu desemba 16,hazijasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza maambukizi ya vorusi vya Corona.

Kuendelea kusambaa kwa virusi hivyo pamoja na vifo kumewafanya viongozi wa nchi kulazimika kurefusha muda wa kufunga shughuli hizo.

Viwango vya maambukizi bado viko juu sana, kutokuwa na uhakika juu ya matokeo ya mkusanyiko wa familia wakati wa sherehe au sikukuu, wasiwasi unaohusiana na aina mpya ya virusi  vya Corona vilivyoanzia kwa mara ya kwanea nchini Uingereza;

Hali ya wasiwasi hospitalini: hizi ni miongoni mwa sababu nyingi ambazo zipelekea Ujerumani inachukua uamuzi wa kuongeza muda wa masharti dhidi ya Corona yanayotumika tangu katikati ya mwezi wa Desemba.Tangu Desemba 29 nchi hiyo imekuwa ikiripoti visa vipya 50,000 vya maambukizi kila siku.Jana Jumatatu nchi hiyo ilirikodi visa 58,784 vya maambukizi mapya kote nchini.

Tangazo la kufungwa shughuli mbali mbali nchini humo limekuja wakati maafisa wa afya wakianza kutoa chanjo ya Oxford-AstraZeneca ambapo ajuza wa miaka 82 alikuwa mtu wa kwanza kupata chanjo.