UFARANSA

Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex aonya kuhusu maambukizi ya Covid 19

Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex
Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex Ludovic Marin/Pool via REUTERS

Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex amesema kuwa mpaka wa nchi yake na Uingereza, utaendelea kufungwa hadi hapo baadaye.

Matangazo ya kibiashara

Aidha, Castex ameeeleza kuwa, juhudi zinafanyika kuongeza kasi ya kutoa chanjo ya kupambana na virusi vya corona.

Katika hatua nyingine, amewataka raia wan chi hiyo kuendelea kuwa macho kwa sababu hali ya maambukizi nchini Ufaransa bado ni mbaya.

“Hakuna shaka kuwa, hatuwezi kulegeza kamba, katika vita dhidi ya Corona,” alisema Castex.

Ufaransa, ilifunga mpaka wake na Uingereza tarehe 20 mwezi Desemba, baada ya nchi hiyo kuripoti aina mpya ya corona na kuzua wasiwasi kuwa hueda maambukizi hayo yakasambaa zaidi.

Waziri wa afya nchini Ufaransa Olivier Veran, amesema kuwa maabara nchini humo yanatumuwa kutambua aina mpya ya virusi hivyo ambavyo vimewaambukiza watu 19.