URUSI

Alexei Navalny kurejea Urusi Januari 17

Alexei Navalny mwanasiasa wa Urusi
Alexei Navalny mwanasiasa wa Urusi AP Photo/Pavel Golovkin

Kiongozi wa upinzani nchini Urusi na mkosoaji mkubwa wa rais wa nchi hiyo Vladimir Putin, Alexei Navalny ambaye anaendelea kupumzika nchini Ujerumani baada ya kupewa sumu aina ya Novichok mnambo mwezi Agosti nchini Urusi, ametangaza kwamba anajiandaa kurejea nchini Urusi siku ya Jumapili.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya kutokuwa na uhakika juu ya hatma yake kuhusiana na kesi yake iliyowasilishwa mahakamani nchini Urusi, na hata usalama wake, amesema ana nia ya kurudi nyumbani.

"Jumapili Januari 17, ninarudi Moscow kwa ndege ya shirika la "Pobeda ", kwa hiyo njoo mnipokee kwa wingi! Alexei Navalny amekamilisha video fupi iliyorushwa kwenye mtandao wa Instagram kwa maneno haya. Video hiyo iliambatanishwa na ujumbe ulioandikwa, ambamo anaeleza sababu za kurudi: "Sijawahi kuulizwa swali la kurudi au la nchini Urusi. Kwa sababu sijaondoka. Nilipelekwa Ujerumani nikiwa katika hali mbaya sana. "

Kulingana na matokeo ya maabara tatu za Ulaya na Shirika la Kupiga marufuku Silaha za Kemikali (OPCW), mpinzani huyo aliwekewa sumu na afisa wa serikali ya Urus, amekumbusha Anastasia Becchio wa kitengo cha Ulaya cha RFI.

Alexei Navalny amebaini kwamba mamlaka ya Urusi inafanya kilio chini ya uwezo wake ili kumzuia asiwezi kurudi nchini Urusi: "Niliponea kuuawa. Na sasa Vladimir Poutine, ambaye aliagiza mauaji yangu [...] anawaambia watumishi wake wafanye kila liwezekanalo ili nisirudi. "

Mwishoni mwa mwezi uliopita, uchunguzi wa "udanganyifu mkubwa" ulifunguliwa dhidi yake. Kulingana na Kamati ya Uchunguzi ya Urusi, Alexei Navalny anashukiwa kutumia pesa kwa matumizi ya kibinafsi kwa karibu euro milioni 4 za michango.

Wiki hii, mahakama ilisajili malalamiko ya kuomba Alexei Navalny apewe adhabu ya kifungo, ombi lililotolewa mwaka 2014. Adhabu hiyo itachunguzwa Januari 29.