WHO

Nchi 50 zakabiliwa na aina mpya ya virusi vya Corona

Mkurugenzi Mkuu WHO  Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkurugenzi Mkuu WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus REUTERS/Denis Balibouse

Idadi ya nchi zinazokabiliwa na aina mpya ya kirusi cha Corona kilichoanzia nchini Uingereza imefikia hamsini na nchi 20 zinakabiliwa na kirusi cha aina hiyo kilichoanzia nchini Afrika Kusini, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Matangazo ya kibiashara

Aina ya tatu ya kirusi cha Corona ambacho Japani ilitangaza Jumapili Januari 10 inaweza kuathiri jibu la kinga na kuna haja ya kuitathimini zaidi, kulingana na WHO, ambayo inabaini katika jarida lake la kila wiki "aina mpya ya Corona inayotia wasiwasi".

"Kadiri virusi vya SARS-CoV-2 vinavyoenea, athari inaendelea kuwa kubwa zaidi katika nchini mbalimbali duniani," inasema WHO.

"Viwango vya juu vya maambukizi vinamaanisha kwamba watu wanapaswa kutarajia hali mbaya zaidi kuibuka."