URUSI-CORONA

Urusi kuanza zoezi la kutoa chanjo kwa raia wiki ijayo

Kirusi cha Corona
Kirusi cha Corona NIAID-RML via AP

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameagiza Jumatano hii, Januari 13 kuzindua chanjo kubwa dhidi ya Corona kwa raia wa nchi hiyo kuanzia wiki ijayo, akisema chanjo iliyotengenezwa na maabara  ya nchi yake ni "bora".

Matangazo ya kibiashara

"Ninaomba kuzindua chanjo kubwa dhidi ya Corona kwa wote kuanzia wiki ijayo," amesema wakati wa mkutano wa serikali ya Urusi kwa njia ya video. "Chanjo ya Urusi ni bora duniani," amesema Putin.

Kwingineko duniani Waziri wa Afya wa Ujerumani, Jens Spahn amesema Ujerumani haitoweza kuondoa hatua zote zilizowekwa kwa ajili ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona mwanzoni mwa mwezi Februari.

Spahn amesisitiza haja ya kuwepo kwa tahadhari zaidi ili kuzuia maambukizi zaidi ya aina mpya ya kirusi kinachosambaa kwa haraka zaidi, huku akisema aitachukua miezi mingine miwili au mitatu zaidi kwa matokeo ya chanjo inayotolewa kuanza kuonekana.

Naye Waziri wa Afya wa Taiwan Chen Shih-chung amesema kuwa kisiwa cha Thailand kimethibitisha wagonjwa wa kwanza waliopata aina ya virusi vya corona vya Afrika Kusini.

Watu hao walikuwa wamesafiri katika nchi jirani ya Eswatini, iliyokuwa ikiitwa zamani kama Swaziland, inayopakana na Afrika Kusini.

Kuanzia Alhamisi, yeyote anayesafiri kwenda Eswatini katika kipindi cha siku 14 atalazimika kwenda karantini katika majengo ya serikali.