ITALIA

Italia yaongeza muda wa vizuizi dhidi ya COVID-19

Waziri Mkuu wa Italia  Giuseppe Conte
Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte REUTERS/Johanna Geron

Kiongozi wa serikali nchini Italia, Giuseppe Conte, ametia saini agizo jipya leo Ijumaa, sheria inayoimarisha hatua za kupunguza janga la Corona, baada ya onyo lililotolewa na Wizara ya Afya kufuatia kuongezeka kwa  hali mbaya ya kiafya.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya kila siku ya visa vipya vya maambukizi ni kati ya 15,000 na 20,000 dhidi ya karibu visa 40,000 katikati ya mwezi Novemba, lakini hali bado ni tete katika hospitali bmbalimbali nchini Italia.

Kati ya watu 400 na 600 wanafariki dunia kutokana na COVID-19 kila siku na serikali inatarajia idadi hiyo kuongezeka.

Siku ya Jumatano, Waziri wa Afya, Roberto Speranza, alizungumza mbele Bunge "juu ya kuongezeka tena kwa ugonjwa huo".

Agizo hilo jipya linaimarisha ya sheria ya kutotoka nje iliyowekwa kote nchini kati ya saa 10 jioni hadi saa 5 asubuhi hadi Machi 5 na imebainisha mfumo wa vizuizi unaotolewa na serikali ya kimkoa kulingana na ukali wa kiwango cha maambukizi.

Kumbi za michezo na mabwawa ya kuogelea vitaendelea  kufungwa kote nchini Italia.