UHOLANZI

Serikali yajiuzulu kufuatia kashfa ya kiutawala

Waziri Mkuu wa Uholanzi  Mark Rutte aliyejiuzulu
Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte aliyejiuzulu REUTERS/Michael Kooren

Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte amewasilisha barua ya kujiuzulu kwa serikali yake Ijumaa hii, Januari 15, 2021. Akiwa madarakani tangu mwaka 2010, aliongoza serikali yake ya tatu mfululizo tangu mwaka 2017. Yeye ni mmoja wa viongozi wa kisiasa wa Ulaya waliodumu madarakani kwa muda mrefu.

Matangazo ya kibiashara

Kujiuzulu huku kulitarajiwa, kwani serikali ya Uholanzi ilikuwa ikijitahidi tangu mwezi Desemba katika kashfa kubwa ambayo maelfu ya familia walishtakiwa vibaya kwa udanganyifu.

“Utawala wa sheria lazima ulinde raia wake kutoka kwa serikali yenye nguvu zote. Ilishindwa kwa njia ya kutisha, ”Mark Rutte amesema katika mkutano na waandishi wa habari, akithibitisha kwamba alikuwa amempa Mfalme Willem-Alexander barua ya kujiuzulu.

Kesi hiyo ilifichuliwa na ripoti ya uchunguzi wa bunge iliyotolewa mnamo mwezi Desemba. Maafisa walisitisha marupurupu ya maelfu ya familia zilizoshutumiwa vibaya kwa udanganyifu kati ya mwaka 2013 na 2019, kabla ya kuwalazimisha kurudisha kwenye hazina ya serikali mabilioni ya fedha walizopokea zaidi ya miaka kadhaa iliyopita, wakati mwingine makumi ya maelfu ya euro.

Jambo ambalo liliziaingiza baadhi ya familia katika shida kubwa za kifedha.

Kwa upande wa wazazi husika 26,000, wamesema hatua hiyo ya kiutawala ilisababisha wengi kufilisika.

Viongozi wakuu wa kisiasa, ikiwa ni pamoja na mawaziri kadhaa walio madarakani, wanashutumiwa kufumbia macho suala ambalo walikuwa wakijua.