UFARANSA

COVID-19 yaendelea kusababisha maafa nchini Ufaransa

Watu wachukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya corona nchini Ufaransa
Watu wachukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya corona nchini Ufaransa REUTERS/Gonzalo Fuentes

Mnamo mwaka 2020, Ufaransa ilirekodi, vifo 53,900 zaidi kuliko mwaka 2019, sawa na zaidi ya 9% ya vifo kutokana na matukio mbalimbali, kulingana na Taasisi ya Takwimu ya Kitaifa na Tathmini ya Kiuchumi (INSEE).

Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa Ufaransa imerekodi vifo 667,400 vilivyotokana na matukio mbalimbali. Kamwe katika historia yake ya hivi karibuni Ufaransa haijarekodi vifo vya juu zaidi kwa kipindi cha mwaka mmoja pekee. Idadi hii ya vifo 53,900 zaidi kuliko mwaka 2018 na 2019, sawa na ongezeko la 9% na bado takwimu zinaweza kukaguliwa tena katika wiki zijazo.

Kama ukuaji wa watu na kuzeeka kunaweza kuelezea sehemu ya rekodi hii ya vifo, janga la COVID-19 lilisababisha idadi ya vifo kuongezeka zaidi katika msimu wa joto na wabaridi. Ufaransa hasa ilirekodi zaidi ya vifo 2,000 kwa karibu kila siku kati ya Machi 16 na Aprili 19.

Kupungua kwa uhalifu na ajali

Licha ya kupungua kwa uhalifu na ajali za barabarani kwa sababu ya vzuizi kwa kudhibiti COVID-19, vifo vingi viliwakumba watu walio na umri wa zaidi ya miaka 65, kwa zaidi ya 10% kulingana na takwimu za INSEE wakati idadi ya vifo imepungua kwa 6% kwa kundi la watu walio chini ya miaka 25.

Data muhimu ya mwisho ni kwamba mikoa ya Ufaransa iliyo na vifo vingi zaidi ni Ile-de-France ikiongoza kwa 18% ya vifo na Grand-Est kwa zaidi ya 13% ya vifo, maeneo mawili yalioathiriwa zaidi na mlipuko wa kwanza wa COVID-19 mwaka 2019.