URUSI

Kiongozi wa upinzani Urusi Alexei Navalny akamatwa baada ya kurejea nchini

Alexei Navalny  mwanasiasa wa upinzani nchini Urusi
Alexei Navalny mwanasiasa wa upinzani nchini Urusi AP Photo/Pavel Golovkin

Mkosoaji mkubwa wa serikali ya Urusi, Alexei Navalny amezuiwa na maafisa wa usalama baada ya kurejea nyumbani, miezi mitano baada ya kuondoka nchini humo kwenda kupewa matibabu nchini Ujerumani baada ya kupewa sumu.

Matangazo ya kibiashara

Mwanaharakati huyo mwenye umri wa miaka 44, alikuwa apokelewe na maefu ya wafuasi wake katika uwanja wa ndege jijini Moscow, akitokea jijini Berlin lakini ndege iliyokuwa imembeba ikaelekezwa katika mji mwingine.

Hatua ya serikali ya Urusi kumkamata, huenda sasa akafungwa jela miaka mitatu na nusukwa kukiuka masharti ya kifungo alichokuwa amepewa akiwa nje ya nchi.

Kukamatwa na kuzuiwa kwa Navalyn kumlaaniwa na Marekani, Ufaransa; Italia na Umoja wa Ulaya, na kutaka kuachiliwa mara moja kwa mwanaharakati huyo.

Navalny ameendelea kuishtumu serikali ya Urusi kwa kumpa sumu kwa lengo la kumuua, madai ambayo hata hivyo yanakanushwa na serikali ya rais Vladimir Putin.