UFARANSA

Mjadala kufanyika katika Bunge kuhusu mpango wa kufufua uchumi wa euro bilioni 750

Rais wa Ufaransa  Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron AP News

Hii ni hatua ya uamuzi kwa mpango wa euro bilioni 750 wa kufufua uchumi wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Kabla ya mataifa 27 kupokea pesa hizi, ambazo zinatarajia kuyawezesha kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi unaosababishwa na janga la COVID-19, Bunge zao zinapaswa kutoa idhni kwa kufadhili mpango.

Nchini Ufaransa, nakala hiyo inachunguzwa katika Bunge la  la nchi hiyo Jumanne hii, Januari 26.

Inaelezwa kuwa euro hizi bilioni 750 zitalipwa kwa sehemu na ushuru mpya wa Umoja wa Ulaya, kwenye shughuli za plastiki au za kifedha. Hli ambayo imzua mjadala mkubwa nchini Ufaransa.

Uholanzi na mataifa mengine pinzani yanataka sehemu kubwa ya fedha za mfuko wa uokozi zisitolewe  kama misaada na badala yake iwe mikopo ambayo nchi wanachama zitakazonufaika zitalazimika kuzilipa miaka michache ijayo.

Wabunge wa Umoja wa Ulaya wanataka mpango utakaopitishwa ujumuishe masharti ya kulinda utawala wa sheria na uwezekano wa kuzuia msaada wa kifedha kwa mataifa wanachama yanayokiuka misingi ya kidemokrasia.