UFARANSA

Ufadhili wa misikiti kutoka nchi za kigeni waibua maswali Ufaransa

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron AP News

Wabunge nchini Ufaransa wanaanza wiki hii uchunguzi wa muswada "wa kuimarisha kanuni za Jamhuri", ambao unaitwa sheria dhidi ya msimamo mkali.

Matangazo ya kibiashara

Muswada huu unakusudia kulinda kanuni ya kutopendelea upande wowote kidini na hii inahusisha hasa ukaguzi wa mashirika Kwa mfano, unayataka mashirika ya kidini kuwa wazi zaidi juu ya sehemu kunakotoka michango yao kutoka nje.

Maeneo ya Waislamu ya ibada yanalengwa na muswada huu. Hali hiyo imezua utata mkubwa hasa katika mji wa Angers, Magharibi mwa Ufaransa Ujenzi wa msikiti mkubwa ulianza miaka mitano iliyopita. Ujenzi wa msikiti huu utakapokamilika, utakuwa msikiti wa 4 nchini Ufaransa, wenye uwezo wa kupokea waumini 2,500.

Thuluthi mbili ya jengo hilo liko chini ya ardhi, ujeshi ambao unaendeshwa kwa misaada kutoka kwa waamini. Lakini kwa kufadhili haraka awamu ya mwisho ya kazi hiyo ya ujenzi, Chama cha Waislamu huko Angers kimekubali ushiriki wa nchi ya Morocco.

Rabat imeahidi kutoa euro milioni 4.5 kwa sharti la kuwa mmiliki wa sehemu hiyo ya ibada, hali ambayo imezua utata.