ITALIA - DRC - USALAMA

Italia yatoa heshima za mwisho kwa balozi Attanasio, aliyeuawa DRC.

Wanajeshi wa Italia wakiwa wamebeba maiti ya balozi Luca Attanasio na mlizi wake Vittoria Lacovacci, waliouawa nchini DRC.
Wanajeshi wa Italia wakiwa wamebeba maiti ya balozi Luca Attanasio na mlizi wake Vittoria Lacovacci, waliouawa nchini DRC. Vincenzo Pinto AFP

Taifa la Italia limetoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa balozi wake nchini Jumhuri ya Kidemokrasia ya Congo , Luca Attanasio na mlinzi wake Vittoria Lacovacci, aliouawa nchini DRC wakiwa katika msafara wa umoja wa mataifa, jumbe za imani kurejea nchini DRC zikishamiri katika ibada hiyo ya mazishi.

Matangazo ya kibiashara

Ibada hiyo imefanyika katika kanisa la Santa Maria degli Angeli basilica, na kuhudhuriwa na waziri mkuu wa Italia, Maria Draghi.

Balozi Attanasio na mlinzi wake waliuawa siku ya jumatatu kaskazini mwa mkowa wa Goma wakati watu wenye silaha walivizia msafara wao, dereva wa shirika la mpango wa chakula la umoja wa mataifa WFP, Moustapha Milambo, pia akiuawa.

Italia tayari imetaka umoja wa mataifa kuunda jopo kuchunguza nini kilitokea hadi waasi wakamuua balozi Attanasio.

Viongozi wa dini waliohudhuria ibada hiyo wametoa wito wa taifa la DRC na mataiafa mengine yanasumbuliwa na waasi ili vita hivyo kusitishwa mara moja.

Balozi Attanasio amemuacha nyuma mjane moja na watoto watatu.