Rais wa Armenia ahidi kutatua mzozo wa kisiasa
Imechapishwa:
Rais wa Armenia, Armen Sargsyan, ameahidi kuchukuwa hatua za dharura kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo, hasa baada ya waziri mkuu, Nikol Pashinyan, kutuhumu jeshi la taifa hilo kuwa lina mpango wa kuipindua serikali.
Rais Armen amesema baadhi ya hatua anazolenga kuchukuwa ni pamoja kupunguza hali ya wasiwasi inayoshuhudiwa kufutia fununu za jeshi kataka kupindua serikali yake, akiongeza kuwa anatafuta njia mwafaka ya kusuluhisha mzozo huo.
Amewataka raia wa taifa hilo, idara za serikali, vikosi ya usalama na wanasiasa, kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuchangia vurugu .
Jeshi nchini Armenia, linamtaka Nikol kujiuzulu kufutia hatua ya Armenia kuonekana kushindwa na taifa la Azerbaijan, kwenye eneo ambalo mataifa hayo mawili yalikuwa yakizozania la Nagorno-Karabakh, hatua anayoiona waziri mkuu Nikol njama ya kupindua serikali.
Waziri mkuu ndiye aliyesaini mkataba
Nikol ndiye aliyetia saini mkataba wa Novemba 10 mwaka uliopita, mkataba ulioipa nguvu taifa la Azerbaijan kudhibiti êneo kubwa la Nagorno-Karabakh, na kulazimisha wanajeshi wa Armenia kuondoka eneo hilo.
Hata hivyo mzozo kati ya jeshi na Nikol, umechochewa na hatua ya Nikol kutaka kumuachisha kazi naibu mkuu wa jeshi nchini humo, kwa kujibu hatua hiyo jeshi lilitoa taarifa likimtaka waziri mkuu kujiuzulu.
Maandamano yamekuwa yakishuhidiwa nchini Armenia,raia wakimtaka waziri huyo mkuu kujiuzulu, huku wengine wakiandamana kupinga kujizulu kwake.