EU-CORONA-AFYA

Viongozi wa Ulaya kujadili kuhusu COVID-19

Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, Brussels, Februari 17, 2021.
Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, Brussels, Februari 17, 2021. REUTERS - POOL

Mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi na serikali wa wanachama wa Umoja wa Ulaya unafanyika leo Alhamisi hii, Februari 25 na kuendelea hadi Ijumaa kwa njia ya video.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo ajenda ya mkutano huo ni kuhusu janga la COVID-19. Kuratibu katika mazingira bora vita dhidi ya ugonjwa huo, "kuongeza" kampeni ya chanjo. Lakini suala hilo limewagawanya viongozi hao.

Kwanza, kuhusu suala la mipaka. Pamoja na kuongezeka kwa idadi ya visa inayohusiana na aina mpya ya kirusi cha Corona, nchi kadhaa ikiwa ni pamoja na Ujerumani, Ubelgiji, Denmark, Finland, Sweden na Hungary zimechukua hatua kali za kufunga mipaka yao kulaaniwa vikali mwanzoni mwa wiki na Tume ya Ulaya kwa sababu ya vizuizi vinavyokiuka uhuru wa kutembea katika nchi za Ulaya.

Mkutano unaofunguliwa Alhamisi hii utakuwa ni fursa kwa viongozi hao kushirikiana pamoja.

Kulingana na serikali ya Uigiriki, mtu yeyote ambaye amepewa chanjo na ambaye ana cheti cha matibabu anapaswa kuwa na haki ya kusafiri kwa kadri anavyoweza ikatika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya. Hadi sasa, viongozi wa umoja huo hawajakubaliana na pendekezo hilo .

Nchi kadhaa wanachama, pamoja na Ufaransa, zinasubiri uthibitisho kwamba chanjo zote zinaweza kuondoa hatari ya maambukizi. Pamoja na dhamana kwa muda wa kinga iliyotolewa na maandalizi ya maabara ya Pfizer, Moderna na AstraZeneca. Lakini wote wanakubaliana kwa suala moja tu: cheti hiki lazima kiendelezwe katika Umoja wa Ulaya ili kuepusha mkanganyiko.