UFARANSA-HAKI

Ufaransa: Kesi nyingine zinazomsubiri Nicolas Sarkozy

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy Novemba 11, 2019.
Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy Novemba 11, 2019. AFP - LUDOVIC MARIN

Mahakama bado inamfuatilia rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy siku moja baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu. Nicolas Sarkozy anatarajia kukata rufaa kwa mahakama mjini Paris  inayojumuisha mwaka mmoja gerezani na miaka miwili ya kifungo cha nje.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu Jumatatu wiki hii baada ya kukutwa na hatia ya ufisadi na kueneza ushawishi.

Sakorzy alikuwa anashtakiwa kwa kujaribu kupata taarifa za ndani kinyume cha sheria kuhusu uchunguzi juu ya ufadhili wa kampeni zake kutoka kwa jaji mwaka 2014. Mahakama hiyo imesema Sarkozy atakuwa na haki ya kuomba kuzuiliwa nyumbani kwa kutumia bangili ya umeme.

Kesi nyingine ya Sarkozy kuanza kusikilizwa

Kesi inayohusiana na akaunti zake za benki kuhusu kampeni yake ya uchaguzi wa urais ya 2012, inayojulikana zaidi kama kesi ya

Nicolas Sarkozy

 Mahakama bado inamfuatilia rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy siku moja baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu.

Nicolas Sarkozy anatarajia kukata rufaa kwa mahakama mjini Paris  inayojumuisha mwaka mmoja gerezani na miaka miwili ya kifungo cha nje.

Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu Jumatatu wiki hii baada ya kukutwa na hatia ya ufisadi na kueneza ushawishi.

Sakorzy alikuwa anashtakiwa kwa kujaribu kupata taarifa za ndani kinyume cha sheria kuhusu uchunguzi juu ya ufadhili wa kampeni zake kutoka kwa jaji mwaka 2014. Mahakama hiyo imesema Sarkozy atakuwa na haki ya kuomba kuzuiliwa nyumbani kwa kutumia bangili ya umeme.

Kesi nyingine ya Sarkozy kuanza kusikilizwa

Kesi inayohusiana na akaunti zake za benki kuhusu kampeni yake ya uchaguzi wa urais ya 2012, inayojulikana zaidi kama kesi ya "Bygmalion" inatarajia kuanza Mars 17. Rais wa zamani anatuhumiwa kufadhili kampeni yake kinyume cha sheria na kuzidi kiwango kilichoidhinishwa cha matumizi ya zaidi ya Euro milioni 20. Anakabiliwa na kifungo cha mwaka mmoja jela.

Kesi nyingine inayomsubiri Nicolas Sarkozy: ile ya ufadhili wa Libya wa kampeni yake ya urais mwaka 2007. Anashukiwa kuwa aliomba serikali ya Muammar Gaddafi pesa na kufadhili kampeni yake ya uchaguzi ili kuweza kuibuka mshindi wa uchaguzi huo. Kwa sasa, Nicolas Sarkozy anashtakiwa kwa ufisadi na kujiunga na wahalifu.

Kesi ya hivi karibuni inahusu shughuli zake za ushauri katika sekta binafsi. Mnamo mwezi Julai mwaka uliyopita, uchunguzi wa awali ulifunguliwa na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka mkuu wa masuala ya fedha kwa biashara ya ushawishi.