UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya visa vipya 11,900 vyaripotiwa nchini Ujerumani

Raia nchini Ujerumani wameendelea kutolewa wito wa kufanya vipimo vya COVID-19>
Raia nchini Ujerumani wameendelea kutolewa wito wa kufanya vipimo vya COVID-19> AFP/Torsten Silz

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 2,471,942, baada ya visa vipya zaidi ya 11,912 kuthibitishwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Alhamisi na taasisi ya udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza nchini Ujerumani ya Robert Koch.

Matangazo ya kibiashara

Taasisi hiyo pia imeripoti vifo vipya 359, na kufikisha jumla ya vifo 71,240 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Baada ya mkutano na viongozi wa majimbo (Länder), Kansela Angela Merkel alitangaza Jumatano jioni kuanza kulegeza hatua kwa hatua makataa yaliyowekwa kwa kudhibiti jana la COVID-19t kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo.

Ujerumani katika miezi ya hivi karibuni ilishuhudia idadi kubwa ya visa vya maambukizi na baadaye kuchukuwa hatua kali ya kukabiliana na ugonjwa huo hatari, ambao umesababisha vifo vingi duniani.