UFARANSA-BRKHANE-USALAMA-DIPLOMASIA

Ufaransa: Mjadala juu ya sera za Ufaransa huko Sahel kufanyika bungeni

Kutumwa kwa wanajeshi wa Ufaransa katika nchi za kigeni Mali Barkhane kimeibua maswali mengi nchini humo>
Kutumwa kwa wanajeshi wa Ufaransa katika nchi za kigeni Mali Barkhane kimeibua maswali mengi nchini humo> © AFP/Dominique Faget

Mjadala kuhusu sera za Ufaransa huko Sahel unafanyika Alhamisi hii, Machi 4 katika Bunge la nchi hiyo. Majadiliano ambayo yatahudhuriwa na Waziri wa Jeshi, Florence Parly.

Matangazo ya kibiashara

Operesheni ya kikosi cha Barkhane inatarajiwa kujadiliwa kwa kina na wabunge nchini Ufaransa, baada ya vyama kadhaa kuomba Bunge kupigia kura kutumwa kwa vikosi vya Ufaransa katika nchi za kigeni.

Ilikuwa Aprili 22, 2013, miezi zaidi ya mitatu baada ya kuzinduliwa kwa Operesheni Serval nchini Mali, wabunge wa Ufaransa waliidhinisha kurefushwa kwa muda wa ujumbe huo wa jeshi. Miaka minane baadaye, Serval ilibadili jina na kuitwa Barkhane, na Bunge halikushauriwa.

Hakika, Katiba hailazimishi. Na hili ni shida, kulingana na mbunge Bastien Lachaud kutoka chama cha  France Insoumise: "Haiwezekani kwamba rais peke yake ndiye anayeamua juu ya kutumwa kwa wanajeshi katika nchi za kigeni na kuwazuia kuendelea kubaki huko. Inasemekana kuwa tayari tumepoteza wanajeshi 55, mamia wengine waliojeruhiwa, Mabilioni kadhaa ya euro, yote kwa hiari ya mtu mmoja, rais, bila mjadala wowote wa kidemokrasia. "

Kura kila miezi mitatu?

Chama cha France Insoumise kinataka kila baada ya miezi mitatu kura ipigwe. Lakini kwa upande Sereine Mauborgne, mbunge kutoka kambi ya walio wengi na afisa wa ujumbe wa kutafuta ukweli wa Bunge juu ya kikosi chaBarkhane, anasema utaratibu huu wa Bunge kutoa uamuzi wake kwa kutuma au kubaki wanajeshi wa Ufaransa katika nchi za kigeni ni mgumu kuanzisha.