UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa vipya 10,580 vyathibitishwa Ujerumani

Ujerumani imeendelea kurekodi visa vingi vya maambuzi ya virusi vya Corona.
Ujerumani imeendelea kurekodi visa vingi vya maambuzi ya virusi vya Corona. REUTERS/Leon Kuegeler

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 2,482,522, baada ya visa vipya 10,580 kuthibitishwa siku moja iliyopita, kulingana na takswimu zilizotolewa leo Ijumaa na taasisi ya magonjwa ya kuambukiza ya nchini Ujerumani Robert Koch (RKI).

Matangazo ya kibiashara

Taasisi hiyo pia imeripoti vifo vipya 264, na kufikisha jumla ya vifo 71,504 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Baada ya mkutano na viongozi wa majimbo (Länder), Kansela Angela Merkel alitangaza Jumatano jioni kuanza kulegeza hatua kwa hatua makataa yaliyowekwa kwa kudhibiti jana la COVID-19t kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo.

Ujerumani katika miezi ya hivi karibuni ilishuhudia idadi kubwa ya visa vya maambukizi na baadaye kuchukuwa hatua kali ya kukabiliana na ugonjwa huo hatari, ambao umesababisha vifo vingi duniani.