NEW ZEALAND-HALI YA HEWA

Onyo la Tsunami lafutwa New Zealand na New Caledonia

Wakazi ambao walihama Pwani ya Papamoa, New Zealand, baada ya onyo la tsunami kusikika Ijumaa Machi 4, 2021 katika eneo la Pasifiki.
Wakazi ambao walihama Pwani ya Papamoa, New Zealand, baada ya onyo la tsunami kusikika Ijumaa Machi 4, 2021 katika eneo la Pasifiki. AP - George Novak

New Zealand imeshusha kiwango chake cha onyo la tsunami, iliyotangazwa baada ya tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 8 kwenye vipimo vya Richter kupiga karibu na Visiwa vya Kermadec karibu na pwani ya kaskazini mashariki suiku ya Alhamisi, shirika la kitaifa la Usimamizi wa Majanga (NEMA) limesema leo Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Mawimbi ya tsunami yenye kasi ndugo yameshuhudiwa na shirika la kitaifa la Usimamizi wa Majanga (NEMA) limesema katika jarida lake kwamba "wakaazi wote wanaweza kurudi nyumbani."

Tahadhari ya tsunami pia imeondolewa huko New Caledonia, Waziri wa Ufaransa mwenye dhamana Outre-mer, Sébastien Lecornu ametangaza kwenye Twitter.

Mapema leo, mamlaka imetoa wito kwa wakaazi kuendelea kuwa waangalifu, na awali shirika la kitaifa la Usimamizi wa Majanga (NEMA) liliwashauri wakaazi wa baadhi ya maeneo ya pwani kuhamia sehemu salama zenye urefu wa juu.