FINLAND

Coronavirus: Uchaguzi wa serikali za mita waahirishwa Finland

Finland imeendelea kurekodi visa vingi vya maambukizi.
Finland imeendelea kurekodi visa vingi vya maambukizi. Lehtikuva/AFP/Archivos

Finland itaahirisha uchaguzi wake wa sewrikali za mitaa uliopangwa kufanyika mwezi ujao hadi katikati ya mwezi Juni. Kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya virusi vya Corona kumezidisha hofu ya uwezekano wa maambukizi zaidi baada ya uchaguzi huo, Waziri wa Sheria ametangaza.

Matangazo ya kibiashara

Finland ni miongoni mwa nchi za Ulaya zilizoathiriwa zaidi na janga hilo lakini mamlaka inasema iko makini kutokana na kuongezeka kwa visa vya maambukizi hivi karibuni na kuibuka kwa aina mpya ya kirusi cha Corona nchini humo, hasa katika mji mkuu wa Helsinki na viunga vyake.

Uchaguzi wa serikali za mitaa ambao ulipangwa kufanyika Aprili 18 hatimaye utafanyika Juni 13, ametangaza Waziri wa Sheria Anna-Maja Henriksson, akionya kuwa uhalali wa uchaguzi huo unaweza kuathiriwa ikiwa watu wengi watakaa nyumbani badala ya kupiga kura.

Finland ina manispaa 309 zinazoendeshwa na mabaraza ambayo hulipa wakaazi na kudhibiti huduma za kimsingi kama huduma ya afya na elimu.

Vyama tisa kati ya 10 hivi sasa katika bunge la Finland vilikuwa vinapendelea kuahirisha uchaguzi wa serikali za mitaa, ispokuwa chama kimoja tu, chama cha mrengo wa kulia dhidi ya Ulaya, kimekua kikitaka uchaguzi ufanyike mwezi ujao kama ilivyopangwa.

Kufikia sasa, Finland imerekodi visa 61,552 vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo 767, na watu 239 wamelazwa hospitalini kwa sababu ya janga hilo.