ULAYA-CHANJO

Kampuni ya AstraZeneca yalemewa kusambaza chanjo barani Ulaya

Chanjo ya  AstraZeneca
Chanjo ya AstraZeneca © Internet

Kampuni ya Uingereza na Sweden inayotengeza chanjo ya AstraZeneca kupambana na maambukizi ya Corona, imetangaza kuwa inakabiliwa na uhaba wa chanjo hiyo kupeleka katika nchi za Umoja wa Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

AstraZeneca inasema inasikitika kuwa inashindwa kusambaza chanjo hiyo katika mataifa ya Ulaya kama ilivyotarajiwa, licha ya juhudi za kutenegeza na kusambaza chanjo hiyo.

Awali, kampuni hiyo ilikuwa imeonya kuwa inakabiliwa na uhaba wa chanjo hiyo barani Ulaya kwa sababu ya changamoto inayoshuhudiwa katika mitambo yake ya uzalishaji.

Katika hatua nyingine, maduka, Mikahawa na Shule zitafungwa kuanzia siku ya Jumatatu wiki ijayo, nchini Italia, baada ya nchi hiyo ya bara la Ulaya kuanza kushuhudia ongezeko la maambukizi ya  virusi vya Corona.

Waziri Mkuu Mario Draghi amesema serikali imelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na mlipuko mpya unaoshuhudiwa nchini humo.

Aidha, kipindi cha pasaka kati ya tarehe 3 hadi 5 mwezi Aprili, nchi hiyo itafungwa kabisa, katika nchi hiyo ambayo imeripoti vifo zaidi ya 100,000 na kuwa taifa la pili kwa vifo barani Ulaya, baada ya Uingereza.

Italia ilikuwa nchi ya kwanza duniani, kufungwa baada ya kuzika kwa maambukizi ya virusi vya corona ambavyo vimewaathiri mamilioni ya watu.