UINGEREZA

Uingereza: Prince Philip aruhusiwa kuondoka hospitalini

Mwanamfalme Philip wa Uingereza anaondoka Hospitali ya King Edward VII.
Mwanamfalme Philip wa Uingereza anaondoka Hospitali ya King Edward VII. REUTERS - PETER CZIBORRA

Mwanamfalme Philip, mume wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza, ameondoka hospitali ya London leo Jumanne ambapo alitibiwa kwa mwezi mmoja, kulingana na shirika la habari la REUTERS likinukuu mwandishi wake.

Matangazo ya kibiashara

Mwanamfalme Phillip wa Uingereza na Mtawala wa Edinburgh alilazwa hospitlia "kama hatua ya kuchukua tahadhari" baada ya kuugua, kulingana nat aarifa ya makao makuu ya Ufalme Buckingham Palace.

Mtawala huyo wa Edinburgh, mwenye umri wa miaka 99, alilazwa katika Hospitali ya King Edward VII mnamo Februari 16 baada ya kujisikia vibaya. Huko alitibiwa kwa ugonjwa wa kuambukizwa, ambayo asili yake haikuelezwa, lakini mbayo hayahusiani na COVID-19.

Alihamishiwa kwa muda mfupi mapema mwezi huu kwatika kituo kingine cha afya cha London kwa operesheni inayohusiana na shida ya moyo iliyokuwepo  wakati analazwa hospitalni kwamara ya kwanza.