UINGEREZA

Coronavirus: Pauni 5,000 kutozwa kwa wanaokwenda likizo kutoka Uingereza

Uingereza inakabiliwa na moja ya ripoti mbaya zaidi ya kibinadamu duniani kutokana na janga hilo, lakini vifo na maambukizi vinapungua haraka na kufanikiwa kwa kampeni ya chanjo kumerejesha imani kwa watu na uchumi.
Uingereza inakabiliwa na moja ya ripoti mbaya zaidi ya kibinadamu duniani kutokana na janga hilo, lakini vifo na maambukizi vinapungua haraka na kufanikiwa kwa kampeni ya chanjo kumerejesha imani kwa watu na uchumi. © AFP/NIKLAS HALLEN

Wasafiri wanaoondoka Uingereza wanaweza katika siku za usoni kutozwa faini ya pauni 5,000 (sawa na euro 5,785) baada ya mpango uliopitishwa ambao unakusudia kupunguza safari zisizo za lazima na kulinda nchi kutokana na maambukizi ya COVID-19 kutoka nje ya nchi.

Matangazo ya kibiashara

Habari hiyo imekatisha tamaa mamilioni ya watu ambao walikuwa na matumaini ya kuondoka wakati wa likizo ya majira ya joto na kusababisha hisa katika sekta ya safari- hasa EasyJet, British AirwayOwner, Jet2 na TUI - kutoka 4.4% hadi 5.3% katikati ya siku.

Uingereza inakabiliwa na moja ya ripoti mbaya zaidi ya kibinadamu duniani kutokana na janga hilo, lakini vifo na maambukizi vinapungua haraka na kufanikiwa kwa kampeni ya chanjo kumerejesha imani kwa watu na uchumi.

Lakini wakati hatua za kulegeza masharti ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona zinatarajia kuanza kutekelezwa mwishoni mwa juma hili, serikali imewaonya raia wake kwamba watalazimika kuachana na likizo zao nje ya nchi.