EU

Nchi za EU zakubaliana kuongeza kiwango cha chanjo ya COVID-19

Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel wakati wa mkutano kwa njia ya video na wakuu wa nchi na serikali kutoka Umoja wa Ulaya, Machi 25, 2021.
Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel wakati wa mkutano kwa njia ya video na wakuu wa nchi na serikali kutoka Umoja wa Ulaya, Machi 25, 2021. REUTERS - YVES HERMAN

Viongozi wa nchi na serikali kutoka Umoja wa Ulaya waliokutana Alhamisi wiki hii kwa mkutano wao wa jadi wamekubaliana kuongeza kutengeneza chanjo ya COVID-19.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video, ulilenga kupata muafaka juu ya kiwango kinachotakiwa kutengenezwa katika umoja huo kwa minajili ya kukidhi mahitaji ya kila nchi wanachama kwa kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya Corona.

Viongozi hao wameonya kuwa wanaweza kuzuia mauzo ya chanjo hizo.

Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel amesema wamekubaliana kuimarisha utoaji wa chanjo hizo kwa nchi wanachama, huku akibaini kwamba ni muhimu kwamba wanaendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kuongeza utengenzaji wa chanjo, wakati ambapo wimbi la tatu la maambukizi ya COVID-19 likiongezeka barani Ulaya.

Wakati huo huo rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen amerejea kuitaka kampuni kubwa ya madawa ya AstraZeneca kuacha kuuza chanjo zilizotengenezwa kwenye nchi za Umoja wa Ulaya.