Covid-19: Ufaransa kukaza masharti ya kukabiliana na maambukizi

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri wa Afya Olivier Véran, Machi 29, 2021 huko Créteil
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri wa Afya Olivier Véran, Machi 29, 2021 huko Créteil AP - Ludovic Marin

Wafaransa natarajia kukabiliana tena na hatua kali kufuatia maamuzi ambayo yatachukuliwa katika kikao cha Baraza la Ulinzi wa Usafi cha kila wiki, kinachoongozwa na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na ambacho kimepangwa kufanyika leo Jumatano Machi 31.

Matangazo ya kibiashara

Hali katika hospitali za Île-de-France inatisha. Masharti rahisi yaliyotangazwa wiki mbili zilizopita yayakuzaa matunda yoyote yaliyotarajiwa kwa visa vya maambukizi na wagonjwa.

Jambo la kanza linalowezekana ni kwamba huenda kusichukuliwi masharti mapya lakini hatua za kupunguza wagonjwa katika wodi za waonjwa mahututi: hatua mpya za kuondoa wagonjwa, kuongeza idadi ya wahudumu wa afya katika wodi mbalimbali, au kuanzisha mpango wa kampeni ya chanjo kwa idadi kubwa ya waalimu.

Jambo lingine linalowezekana: kufungwa kwa shule. Na jambo la tatu linalowezekana: kufungwa kwa shule na watu kuwekewa masharti ya kutembea.

Olivier Véran, Waziri wa Afya, amebaini kwamba serikali "haitawaacha madaktari wawe kwenye nafasi ya kuwabagua wagonjwa"