UINGEREZA

Uingereza yaomboleza kifo cha Mwanamfalme

Mwanamfalme Philip,  Oktoba 2018.
Mwanamfalme Philip, Oktoba 2018. AP - Alastair Grant

Mwanamfalme Philip, Duke (Mtawala) wa Edinburgh. amefariki akiwa na miaka 99, Kasri la Buckingham limetangaza katika taarifa leo Ijumaa Mwanamfalme Philip, Duke (Mtawala) wa Edinburgh. amefariki akiwa na miaka 99, Kasri la Buckingham limetangaza katika taarifa leo Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anasema ni "kwa huzuni kubwa" kupokea habari za kifo cha Mwanamfalme Philip kutoka Kasri la Buckingham.

Akitoa salamu zake za rambirambi alisema Mwanamfalme Philip alipata mapenzi ya vizazi nchini Uingereza, katika Jumuiya ya Madola na ulimwenguni kote.

Boris Johnson amesema kwamba Familia ya Kifalme wamepoteza "sio tu mtu anayependwa sana na anayeheshimiwa sana na umma, lakini mume aliyejitolea, baba mwenye fahari na mwenye upendo, babu, na katika miaka ya hivi karibuni, babu-mkubwa".

Viongozi mashuhuri duniani wa sasa na waliostaafu wanaendelea kutoa salamu zao za rambirambi, wakimwelezea marehemu kama mtu aliyeutumikia Ufalme wa Uingereza kwa juhudi na uadilifu. Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema Hayati Philip alijipatia heshima kubwa nchini Uingereza, katika Jumuiya ya Madola na kwingineko duniani.

Mwanamfalme Philip, amefariki dunia leo Ijumaa akiwa na umri wa miaka 99. 

Kifo chake kimekuja miezi michache tu kabla ya kusherehekea 100 ya kuzaliwa kwake Juni – hafla ambayo kawaida huadhimishwa Uingereza kwa ujumbe wa salamu za pongezi kutoka kwa malkia, ambaye sasa ndiye mtawala wa kifalme aliyehudumu kwa muda mrefu Zaidi Uingereza.