UINGEREZA

Mume wa Malkia wa Uingereza Elizabeth wa pili, azikwa

Msafara uliobeba mwili wa Uingereza Prince Philip, aliyezikwa Aprili 17 2021 jijini London
Msafara uliobeba mwili wa Uingereza Prince Philip, aliyezikwa Aprili 17 2021 jijini London REUTERS - POOL

Prince Philip, mume wa Malkia wa Uingereza Elizabeth wa Pili, aliyefariki dunia tarehe tisa mwezi Aprili akiwa na umri wa miaka 99, amezikwa katika eneo la Windsor Castle, Magharibi mwa jiji la London.

Matangazo ya kibiashara

Amezikwa baada ya dakika 50 za ibada iliyohudhuriwa na watu waombolezaji 30 na familia ya Kifalme akiwemo Malkia Elizabeth wa Pili.

Mikusanyiko ya watu ilizuiwa kwa sababu ya Janga la Covid 19.

Prince Philip na mkewe, walikuwa katika ndoa kwa zaidi ya miaka 70.

Zaidi ya wanajeshi 730 walishiriki katika tukio hilo.