UINGEREZA

Mwanamfale Philip azikwa kwa heshima za kifalme

Wajumbe wa familia ya kifalme watembea nyuma ya gari linalobebamwili wa mwanamfalme Philip, mume wa Malkia Elizabeth II, aliyeaga dunia akiwa na umri wa miaka 99, huko Windsor, Uingereza Aprili 17, 2021.
Wajumbe wa familia ya kifalme watembea nyuma ya gari linalobebamwili wa mwanamfalme Philip, mume wa Malkia Elizabeth II, aliyeaga dunia akiwa na umri wa miaka 99, huko Windsor, Uingereza Aprili 17, 2021. REUTERS - POOL

Mwanamfalme Philip, Mtawala wa Edinburg amezikwa leo Jumamosi katika mazishi ya kifamilia baada ya misa ya kumuombea hayati iliyofanyika katika kanisa la St George.

Matangazo ya kibiashara

Mazishi hayo yameendeshwa kwa taratibu tofauti kwa zingatio la vizuizi vya kupambana na janga la virusi vya Corona. Shughuli hiyo ambayo imehudhuriwa na wanafamilia 30 tu, imeoneshwa moja kwa moja kupitia televisheni mbalimbali, katika kanisa la Mtakatifu George, magharibi mwa London.

Raia wa Uingereza walinyamaza kimya kwa dakika moja ikiwa ishara ya kutoa heshma zao za mwisho kwa mwanamfalme huyo wakati jeneza likiwa njiani kuelekea kanisani.

Jeneza lake lilibebwa kwa mwendo mfupi hadi kanisa la St George kwa kutumia gari aina ya Land Rover au Defender T130, ambalo mtaalamu huyo alichangia katika kulifanyia marekebisho ya muundo wake.

Mwanamfalme Phillip, aliyekuwa mume wa Malkia Elizabeth kwa takribani miaka 73, alifariki Aprili 9 akiwa na umri wa miaka 99.