MYANMAR

Borrell: EU imechukua vikwazo vipya dhidi ya Myanmar

Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel, na Mwakilishi Mkuu wa EU katika Masuala ya Kigeni, Joseph Borell, wanahudhuria mkutano kwa nia ya video na wakuu wa nchi na serikali 27 wa Umoja wa Ulaya, Machi 10, 2020.
Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel, na Mwakilishi Mkuu wa EU katika Masuala ya Kigeni, Joseph Borell, wanahudhuria mkutano kwa nia ya video na wakuu wa nchi na serikali 27 wa Umoja wa Ulaya, Machi 10, 2020. Stephanie Leqocq/Pool via REUTERS

Umoja wa Ulaya umepitisha vikwazo vipya dhidi ya Myanmar kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya Februari 1, Josep Borrell amesema Jumatatu wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

"Tumepitisha kifungu cha pili cha vikwazo, vikubwa zaidi, vinavyolenga watu 10 na makampuni mawili ya kiuchumi ya jeshi", amesema msemaji sera za mambo ya nje za Umoja wa Ulaya wakati wa mkutano na waandishi wa habari kando na mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kutoka kambi hiyo huko Brussels.

Umoja wa Ulaya tayari ulikuwa imeweka vikwazo mnamo mwezi Machi dhidi ya watu 11 waliohusika katika jarbiola mapinduzi.

Umoja wa Ulaya pia umetangaza vikwazo vya silaha dhidi ya Myanmar na inashikilia vikwazo dhidi ya maafisa kashaa wa jeshi la Myanmar tangu 2018.

Myanmar imetumbukia katika machafuko tangu jeshi la jeshi hiyo lilipomkamata Aung San Suu Kyi, kiongozi wa chama cha National League for Democracy (NLD), ambaye chama chake kilishinda uchaguzi uliopita wa mwezi Novemba 2020.