EU

EU yalaani uamuzi wa Moscow wa kufukuza wanadiplomasia 20 wa Jamhuri ya Czech

Wanadiplomasia wa Jamhuri ya Czec waliofukuzwa na Urusi, wakiwasili kwenye uwanaja wa Vaclav Havel huko Prague, aprili 19, 2021.
Wanadiplomasia wa Jamhuri ya Czec waliofukuzwa na Urusi, wakiwasili kwenye uwanaja wa Vaclav Havel huko Prague, aprili 19, 2021. REUTERS - DAVID W CERNY

Umoja wa Ulayaunasikitishwa na uamuzi wa Urusi wa kuwafukuza wanadiplomasia 20 wa Jamhuri ya Czech na inaunga mkono kikamilifu Jamhuri ya Czech, Tume ya Ulaya imesema katika taarifa iliyotolewa Jumatatu jioni.

Matangazo ya kibiashara

"Umoja wa Ulaya una wasiwasi juu ya tabia mbaya za Urusibarani Ulaya," amesema.

"Urusi lazima isitishe shughuli hizi, ambazo zinakiuka kanuni na viwango vya kimataifa vilivyowekwa na kutishia utulivu barani Ulaya," umoja huo imeongeza.

Mapema jana, Prague ilisema iliona majibu ya Moscow kwa mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili "kupindukia".

Urusi iliwafukuza wafanyakazi wa ubalozi wa Jamhuri ya Czech huko Moscow baada ya Jamhuri ya Czech kushtumu idara ya ujasusi ya Urusi kwa kuhusika katika mlipuko wa ghala la silaha mwaka 2014 na kuwafukuza wanadiplomasia 18 wa Urusi.