CHINA

China yalaumu Australia kwa 'mawazo ya vita baridi'

Mahusiano ya kidiplomasia kati ya Australia na China yameharibika tangu Canberra ilipendekeza uchunguzi wa kimataifa juu ya chanzo cha Corona , na kusababisha ulipizaji wa kisasi kuhusiana na biashara kutoka Beijing.
Mahusiano ya kidiplomasia kati ya Australia na China yameharibika tangu Canberra ilipendekeza uchunguzi wa kimataifa juu ya chanzo cha Corona , na kusababisha ulipizaji wa kisasi kuhusiana na biashara kutoka Beijing. © afp.com/FREDERIC J. BROWN

Australia imesema leo Alhamisi kuwa imefuta mikataba miwili na Beijing kuhusiana na mradi wa China wa ujenzi wa barabara mpya "New Silk Road" kwa sababu haukuendana na sera ya kigeni ya serikali ya shirikisho na lengo lake la ukanda wa Indo-Pacific "huru na wazi".

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China ameijibu kwa kushutumu "mawazo ya vita baridi" ya Canberra na "upendeleo wake wa kiitikadi" na kuitaka "irekebishe mara moja makosa yake kwa kurejelea uamuzi wake."

Ubalozi wa China hapo awali ulitaja uamuzi wa Waziri wa Mambo ya nje wa Australia Marise Payne wa kupiga kura ya turufu makubaliano mawili yaliyotiwa saini na jimbo la Victoria kama "ya uchokozi", ikisema kuwa yatazidi kuharibu uhusiano kati yao.

Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison amewaambia waandishi wa habari leo Alhamisi kwamba makubaliano hayo yalifutwa kwa sababu serikali yake ya shirikisho haikutaka serikali za majimbo ya Australia ziingie mikataba inayokinzana na sera ya mambo ya nje ya nchi hiyo.

Mahusiano ya kidiplomasia kati ya Australia na China yameharibika tangu Canberra ilipendekeza uchunguzi wa kimataifa juu ya chanzo cha Corona , na kusababisha ulipizaji wa kisasi kuhusiana na biashara kutoka Beijing.