IRAN-MAREKANI

Mpango wa yuklia wa Iran: Washington na Tehran waendekea kutafautiana

Maafisa wa polisi wakitoa ulinzi nje ya hoteli ambapo mkutano wa Tume ya Pamoja ya Mpango wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA), au mpango wa nyuklia wa Iran, unafanyika, Vienna, Austria, Aprili 20, 2021.
Maafisa wa polisi wakitoa ulinzi nje ya hoteli ambapo mkutano wa Tume ya Pamoja ya Mpango wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA), au mpango wa nyuklia wa Iran, unafanyika, Vienna, Austria, Aprili 20, 2021. © REUTERS/Leonhard Foeger

Marekani na Iran zinaendelea kutofautiana kuhusu jinsi zinaweza kuanza tena kuheshimisha makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015, licha ya maendeleo kadhaa yaliyopatikana katika mazungumzo ya hivi karibuni ya moja kwa moja huko Vienna, amesema afisa mwandamizi wa Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuchukua duru kadhaa, na matokeo yake bado hayajafahamika, afisa huyo mwandamizi kutoka wizara ya mambo ya nje amewaambia waandishi wa habari katika mkutano kwa njia ya simu.

Tofauti kuu zinahusu vikwazo ambavyo Marekani itahitaji kuondoa na kuhusu hatua ambazo Iran itahitaji kuchukua ili kukidhi majukumu ya kupunguza mpango wake wa nyuklia, afisa huyo amesema, huku akitaka jina lake lisitajwe.'

"Bado kuna tofauti, na wakati mwengine, tofauti kubwa, amesema. Hatuko karibu kuhitiisha mazungumzo haya. Matokeo bado hayajajulikana. Lakini kuna "hatua kubwa ambayo imepigwa", ameongeza."

Mazungumzo yataanza tena wiki ijayo.