UFARANSA

Covid-19 Ufaransa: Macron atangaza kulegezwa kwa vizuizi kwa hatua

Rais Emmanuel Macron katika Ikulu ya Elysée, Aprili 29, 2021.
Rais Emmanuel Macron katika Ikulu ya Elysée, Aprili 29, 2021. AP - Lewis Joly

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza kufunguliwa tena kwa nchi hiyo kwa hatua baada ya kufungwa kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa ametangaza mpango wake wa kuondoa vizuizi vya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona hatua kwa hatua. Hayo ameyasema katika vyombo vya habari vya kimkoa Alhamisi wiki hii.

Ametangaza kufunguliwa mikawa, majumba ya sinema, makumbusho, nyumba za sanaa na maktaba zitafunguliwa kuanzia Mei 19, na muda wa kutotembea usiku utapunguzwa hadi saa 3:00 usiku , kabla yakuondolewa kwa hatua Juni 30 kulingana na hali ya kiafya nchini.

Emmanuel Macron ametangaza kalenda ya kuondoa vizuizi hatua kwa hatua katika hatua nne, kuanzia Mei 3 hadi Juni 30, katika mahojiano na vyombo vya habari vya kila vya kimkoa ambayo yamechapishwa Alhamisi, Aprili 29.

Jumatatu ijayo, Mei 3, watu wataruhusiwa kusafiri umbali wa kilomita 10 kutoka nyumba. Shule pia zinatarajia kufunguliwa.