UINGEREZA

Uingereza kuwa mwenyeji wa mkutano wa chanjo mwaka 2022

Matt Hancock, Waziri wa Afya wa Uingereza.
Matt Hancock, Waziri wa Afya wa Uingereza. REUTERS - POOL

Uingereza imesema leo Ijumaa kuwa  itakuwa mwenyeji wa mkutano mwaka 2022 kutafuta pesa za utafiti wa chanjo na maendeleo kusaidia muungano wa kimataifa unaohitaji kuharakisha uzalishaji wa chanjo dhidi ya magonjwa yajayo.

Matangazo ya kibiashara

Uingereza inatumia uenyekiti wakewa Kundi la Mataifa tajiri (G7) ili kusisitiza hitaji la kujiandaa kwa magonjwa ya mlipuko ya baadaye, kwa kuzingatia matokeo mabaya ya mgogoro wa kiafya uliosababishwa na COVID-19.

Uingereza imesema mkutano huo ulioandaliwa na Coalition for Epidemic Preparedness Innovations (CEPI) utasaidia lengo la taasisi hiyo la kupunguza muda wa maendeleo kwa chanjo mpya hadi siku 100 katika magonjwa ya mlipuko ya baadaye.

"Tunatarajia kufanya kazi na CEPI kuharakisha maendeleo ya chanjo, na kutafuta suluhisho la dunia ambalo litawezesha kujiandaa vyema kwa magonjwa ya mlipuko ya baadaye," amesema Matt Hancock, Waziri wa Afya wa Uingereza.

Mkutano huo unakusudia kupata uwekezaji kutoka kwa jamii ya kimataifa, ingawa hakukuwa na habari ya haraka juu ya ni serikali gani au mashirika gani yataalikwa kuhudhuria mkutano huo.