UINGEREZA-G7

G7 kujadili hatua ya uamuzi dhidi ya vitisho vya China na Urusi

Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza Dominic Raab akizungumza na Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken huko Carlton Gardens kabla ya mikutano ya wiki hii ya G7 huko London, Uingereza Mei 3, 2021.
Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza Dominic Raab akizungumza na Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken huko Carlton Gardens kabla ya mikutano ya wiki hii ya G7 huko London, Uingereza Mei 3, 2021. REUTERS - POOL

Uingereza itatafuta Jumanne hii kukubaliana na washirika wake wa G7 juu ya hatua madhubuti za kulinda demokrasia dhidi ya vitisho vya dunia kama vile vinavyotolewa na China na Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya pili ya mkutano wa mawaziri wa kigeni wa G7 huko London unaoandaa mkutano wa mwezi ujao, waziri wa mambo ya nje wa Uingereza ataongoza mazungumzo kuhusu vitisho kwa demokrasia, uhuru na haki za binadamu.

"Uenyekiti wa Uingereza wa G7 ni fursa ya kuleta pamoja jamii zilizo wazi na za kidemokrasia, na kuonyesha umoja wakati ambapo hii inahitajika kweli kujibu changamoto za pamoja na vitisho vinavyozidi kuongezeka," Dominic Raab amesema katika taarifa.

Australia, India, Afrika Kusini na Korea Kusini kushiriki mkuatano wa G7

Mbali na wanachama wengine wa G7 (Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japani, Marekani), Uingereza wiki hii ilialika mawaziri wa mambo ya nje wa Australia, India, Afrika Kusini na Korea Kusini.

Mkutano huo, wa kwanza kufanyika kwa miaka miwili, unaonekana na London kama fursa ya kuunga mkono mfumo wa kimataifa unaohusu sheria dhidi ya kile inachokiona kama majaribio ya Beijing, kupitia ushawishi wake wa kiuchumi, na Moscow, kupitia shughuli zake mbaya, ili kudhuru mfumo huu.

G7 kuijadili Burma

Kwenye orodha ya majadiliano Jumanne hii pia litakuwa swali la Burma, na mwito wa hatua kali zaidi dhidi ya uongozi wa kijeshi ambao ulichukua madaraka mapema Februari kupitia mapinduzi ya kijeshi.