UFARANSA-AFYA

Karantini ya lazima kuingia Ufaransa yaongezwa kwa nchi mpya saba

Wasafiri kutoka nchi saba, ikiwa ni pamoja na Uturuki, watalazimika kuingia karantini ya lazima ya siku kumi baada ya kuwasili Ufaransa
Wasafiri kutoka nchi saba, ikiwa ni pamoja na Uturuki, watalazimika kuingia karantini ya lazima ya siku kumi baada ya kuwasili Ufaransa AFP - ERIC PIERMONT

Wasafiri kutoka nchi saba, ikiwa ni pamoja pamoja na Uturuki, watalazimika kuingia karantini ya lazima ya siku kumi wakati wa kuwasili nchini Ufaransa kwa sababu ya kusambaa kwa janga la COVID-19 katika nchi hizi, chanzo cha serikali kimeliambia shirika la habarila AFP leo Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Kizuizi hiki kitatumika pia kwa Bangladesh, Sri Lanka, Pakistan, Nepal, Falme za Kiarabu na Qatar. Hatua hiyo itaanza kutumika Jumamosi usiku wa manane, baada ya kuchapishwa Jumamosi asubuhi agizo linalohusiana, chanzo hicho kimesema.

Kwa sasa, nchi tano zilikuwa chini ya karantini tangu Aprili 24: Brazil, India, Chile, Afrika Kusini na Argentina.

Wasafiri kutoka nchi hizo lazima watoe uthibitisho wakati wa kuwasili ncini Ufaransa kwa vipimo vya PCR chini ya masaa 36.

Atakayekadi atatozwa faini ya euro 1,000 hadi 1,500

Abiria lazima watangaze kwa ndege mahali pao pa kujitenga nchini Ufaransa, wakisaidia nyaraka. Walakini, karantini hii inaambatana na ruhusa ya kuondoka kati ya saa 10 asubuhi na 12 jioni.

Mtu yeyote atatozwa faini ya euro 1,000 hadi 1,500 ikiwa atarudi kosa. Msemaji wa serikali ya Ufaransa Gabriel Attal alisema Jumatano kuwa "kaguzi 1,500" tayari zimefanywa "kwa watu walio karantini na watu 141 walipigwa faini".

"Lazima tuwe macho sana dhidi ya aina hizi za virusi vipya," alisema.

Hatua hizi mpya zinakuja wakati janga linaendelea kushika kasi nchini India, ambapo wiki hii imerekodi karibu nusu ya visa vya dunia, na katika nchi jirani.