EU

Macron aomba mshikamano wa kijamii kwa nchi za Umoja wa Ulaya

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mkutano na waandishi wa habari kando ya mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa EU uliofanyika Palacio de Cristal huko Porto, Ureno Mei 8, 2021.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mkutano na waandishi wa habari kando ya mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa EU uliofanyika Palacio de Cristal huko Porto, Ureno Mei 8, 2021. REUTERS - POOL

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa wito kwa nchi za Ulaya kuunga mkono mshikamano wa kijamii katika nchi hizo katika mkutano uliopangwa kuhusiana na suala hilo huko Porto, Ureno, licha ya kusita kwa nchi zingine kutoa mfano wao wa kinga au mifumo yao rahisi zaidi inayopaswa kuvutia biashara.

Matangazo ya kibiashara

Wakuu wa nchi na Serikali  ishirini na saba wanatarajia kujadili hasa  maswala ya mshahara wa kutosha kwa Umoja wa Ulaya, kazi au haki za wafanyikazi kwenye makampuni ya dijiti.

Ikiwa mikataba ya Umoja wa Ulaya haiwezeshi mshahara wa chini kuwekwa katika kiwango cha nchi wanachama wa umoja huo, mazungumzo yatahusu ufafanuzi wa vigezo vya kawaida kufafanua katika kila nchi kiwango cha chini cha ujira ili kuepusha tofauti kubwa sana.

Kwenye swali hili, "nchi nyingi zinaonekana kusita, mifano ambayo ni tofauti lakini mfumo unaendelea na kuna nakala ambayo inatambua haj hii ya kuungana," amesema Emmanuel Macron, wakati Ufaransa itachukua uenyekiti wa Umoja wa Ulaya katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2022.