ITALIA

Zaidi ya wahamiaji 400 wawasili Lapeduza Italia

Wahamiaji wanaonekana baada ya kushukakwenye boti ya mbao kwenye kisiwa cha Lampedusa, Italia Oktoba 18, 2019.
Wahamiaji wanaonekana baada ya kushukakwenye boti ya mbao kwenye kisiwa cha Lampedusa, Italia Oktoba 18, 2019. REUTERS - GUGLIELMO MANGIAPANE

Boti nne zilizowabeba zaidi ya wahamiaji 400 zimewasili katika  Kisiwa cha Lampedusa, chini Italia baada ya kukamatwa na mamlaka ya Italia katika eneo hilo la pwani ya Bahari ya Mediterania

Matangazo ya kibiashara

Kulingna na shirika la habari la Italia ANSA, moja kati ya boti hizo, iliyowapakia watu 325, ilizuiwa umbali wa mile 8 kutoka Lampedusa.

Boti nyingine ikiwa na watu 90 ilikamatwa na polisi inayodhibiti ukwepaji wa kodi sambamba na yongine mbili, moja ikiwa na abiria 98 na nyingine watu 16.

Kisiwa cha Lampedusa kimekuwa eneo kuu la kuingilia Ulaya kwa wahamiaji wengi na hasa kutoka katika mataifa ya Tunisia na Libya.