UFARANSA-AFYA

COVID-19: Watu milioni 20 wapokea dozi ya kwanza ya chanjo nchini Ufaransa

Raiw wa Ufaransa Emmanuel Macron Aprili 27, 2021, Elysée.
Raiw wa Ufaransa Emmanuel Macron Aprili 27, 2021, Elysée. © RFI/Pierre René-Worms

Watu milioni ishirini wamepokea dozi yao ya kwanza ya chanjo ya COVID-19 nchini Ufaransa, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza katika ujumbe wa Twitter Jumamosi hii, akiruhusu serikali kufikia lengo ambalo imejiwekea.

Matangazo ya kibiashara

"Watu milioni 20 wa Ufaransa walichanjwa!" Waziri Mkuu Jean Castex pia ameandika kwenye mitandao ya kijamii.

"Kwa wale wote ambao wamehamasishwa kufikia lengo hili: asante kwa kujitolea kwenu na uhamasishaji wenu wa kipekee. Kwa Wafaransa wenzetu ambao bado hawajapata chanjo:mjihimize kwenda kupata chanjo", ameongeza.