UINGEREZA-USHIRIKIANO

Malkia Elizabeth II kumpokea Joe Biden mnamo Juni 13 Windsor

Malkia wa Uingereza Elisabeth II anatarajia kumpokea rais wa Marekani Joe BIden Juni 13.
Malkia wa Uingereza Elisabeth II anatarajia kumpokea rais wa Marekani Joe BIden Juni 13. © AFP

Malkia wa Uingereza Elizabeth II atampokea Rais wa Marekani Joe Biden na mkewe Jill Biden katika kasri la kifalme la Windsor Castle kando ya mkutano wa mataifa Saba muhimu yalioendelea zaidi kiviwanda Juni 13, msemaji wa kasri kifalme ya Buckingham amesema leo Alhamisi.

Matangazo ya kibiashara

Joe Biden atakuwa Rais wa 13 wa Marekani ambaye Mfalme huyo wa miaka 95 atakutana naye tangu kuanza kwa utawala wake mwaka wa 1952.

Kwa malkia, hii itakuwa tukio kuu la kwanza kwenye ajenda yake tangu kifo cha mumewe, Prince Philip, mwezi Aprili.

Uingereza itakuwa mwenyeji wa mkutano wa wakuu wa nchi na serikali kutoka kundi la mataida 7yaliyostawi zaidi kiviwanda, G7 kuanzia Juni 11 hadi 13 huko Carbis Bay, huko Cornwall, ikiwa ni mmoja ya mikutano mikubwa ya kwanza ya kidiplomasia "ana kwa ana" tangu kuzuka kwa janga la COVID-19.

Joe Biden, kwa mkutano huo atafanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu aingie madarakani mwezi Januari mwaka huu.

Pia atasafiri kwenda Brussels Juni 14 kwa mkutano wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi, NATO, na kisha mkutano wa Umoja wa Ulaya (EU) na Marekani Juni 15.