FACEBOOK-UCHUNGUZI

Facebook yalengwa na uchunguzi wa Umoja wa Ulaya na Uingereza

"Kufuatia uchunguzi wa kina, Tume inahofia kuwa Facebook inaweza kupotosha ushindani katika sekta ya huduma za matangazo mkondoni" na kwa hivyo "imefungua utaratibu rasmi wa uchunguzi", imeelezwa katika taarifa kwa waandishi wa habari kutoka kwa Tume ya Umoja wa Ulaya.
"Kufuatia uchunguzi wa kina, Tume inahofia kuwa Facebook inaweza kupotosha ushindani katika sekta ya huduma za matangazo mkondoni" na kwa hivyo "imefungua utaratibu rasmi wa uchunguzi", imeelezwa katika taarifa kwa waandishi wa habari kutoka kwa Tume ya Umoja wa Ulaya. Olivier Douliery AFP/Archivos

Mamlaka ya ushindani ya Umoja wa Ulaya na Uingereza leo Ijumaa imezindua uchunguzi juu ya uwezekano wa tabia ya ushindani wa Facebook katika tasnia ya matangazo mkondoni.

Matangazo ya kibiashara

Tafiti hizi zitatafuta kujua ikiwa mtandao mkubwa wa kijamii unatumia data ya mtumiaji na data iliyokusanywa kutoka kwa wafanyabiashara milioni saba ambao hutangaza kwenye huduma yake ya Soko la Facebook (Marketplace) kushiriki katika masuala ya ushindani.

Kufunguliwa kwa uchunguzi huu wa kwanza kwa Tume dhidi ya Facebook kunakuja pamoja na kesi zingine zilizoanzishwa na Margrethe Vestager, Makamu wa Rais Mtendaji wa Tume ya Ulaya na anayesimamia sera ya mashindano, dhidi ya ùakampuni ya dijiti ya Marekani.

Tume ya Umoja wa Ulaya tayari imetoza faini ya euro bilioni 8 kwa Google, kampuni tanzu ya Alfabeti, na pia inachunguza mitandao ya Amazon na Apple.