G7-USHIRIKIANO

G7: Paris, Berlin, Madrid na Roma watoa kwa makubaliano juu ya kodi ya kimataifa

Waziri wa Fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire.
Waziri wa Fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire. Eric Piermont AFP/Archivos

Mawaziri wa fedha kutoka Ujerumani, Uhispania, Ufaransa na Italia wameomba katika mahojiano yaliyorushwa Ijumaa ili mkutano wa mawaziri wa fedha wa G7 ambao unafunguliwa leo jijini London, nchini Ungereza ufikie makubaliano juu ya kodi ya kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

"Ni wakati muafaka wa kupata makubaliano juu ya suala hili", amebaini Waziri wa Uchumi na Fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire na wenzake wa Ujerumani Olaf Scholz, Uhispania Nadia Calviño na Italia Daniele Franco katika nakala hii iliyochapishwa na Gazeti la kila siku la Uingereza The Guardian

"Nafasi ya kufikia makubaliano iko karibu, wacha tuitumie", pia amehimiza Bruno Le Maire kwenye mtandao wa Twitter leo Ijumaa.

"Natoa wito kwa nchi zote za G7 kuunga mkono makubaliano ya ulimwengu juu ya kodi ya dijiti na kodi ya chini katika mkutano uliofanyika London leo Ijumaa. Hii ni hatua ya uamuzi kabla ya mkutano wa nchi za G20 mwezi Julai," ameongeza waziri huyo wa Ufaransa, mtetezi wa muda mrefu wa makubaliano ya kimataifa juu ya kodi ya chini ya makampuni na kodi ya makampuni makubwa ya kidijitali.