UFARANSA

Emmanuel Macron azabwa kofi wakati wa ziara yake kusini mwa Ufaransa

Emmanuel Macron wakati wa ziara yake katika shule ya hoteli huko Tain-l'Hermitage, kabla ya kuzabwa kibao, mnamo Juni 8, 2021.
Emmanuel Macron wakati wa ziara yake katika shule ya hoteli huko Tain-l'Hermitage, kabla ya kuzabwa kibao, mnamo Juni 8, 2021. REUTERS - POOL

Rais wa Ufaransa Emmanuel amepigwa kofi na mwanamume mmoja wakati wa ziara yake kusini mashariki mwa nchi hiyo. Video ya tukio hilo imemuonyesha mwanamume mmoja aliyekuwa miongoni mwa watu akimzaba kibao rais Macron.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hili limetokea wakati Macron alipolitembelea eneo la Drome mashariki mwa Ufaransa ambako alikutana na wamiliki wa migahawa na wanafunzi kuzungumza nao kuhusu jinsi maisha yanavyorejea hali ya kawaida baada ya janga la Covid-19.

Kwenye video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Bwana Macron anaonekana akitembea kwenda kwa kizuizi katika safari ya kwenda Tain-l'Hermitage nje ya jiji la Valence.

Ziara yake katika eneo hilo ilipangwa kuendelea Jumanne, maafisa walisema, na safari ya taasisi ya ufundi kwa vijana walio na miaka umri wa miaka 25-30.

Ofisi ya rais imesema pamefanyika jaribio la kushambulia Macron lakini haikutoa taarifa zaidi.

Waziri Mkuu Jean Castex aliliambia Bunge la taifa muda mfupi baadaye kwamba wakati demokrasia ilimaanisha mjadala na kutokubaliana kwa njia halali "lazima iwe kwa vyovyote vile haina maana ya vurugu, uchokozi wa maneno na hata shambulio la kujeruhi".

Kiongozi wa mrengo wa kushoto Jean-Luc Mélenchon aliandika katika twitter "mshikamano na Rais" mara tu baada ya kiongozi huyo kushambuliwa kwa kofi .

Marine Le Pen ametangaza kwa waandishi wa habari: "Mimi ni mpinzani wa kwanza wa Emmanuel Macron, lakini yeye ni Rais wa Jamhuri na kwa hivyo, tunaweza kukabiliana naye kisiasa, lakini hatuwezi kukabilina kwa njia yoyote ya kumshambulia, au kumletea vurugu. Tabia hii haikubaliki na inalaaniwa vikali katika demokrasia. "

Xavier Bertrand, kiongozi wa zamani wa LR wa amelaani "kitendo kisichookubalika". “Mgawanyiko wa kisiasa haumaanishi vurugu. "